Afya

Utafiti:Tambua jinsi ya kuepuka kuumwa na mbu

Tarehe January 31, 2018

Watafiti wa masuala ya biolojia kutoka Marekani wamebaini kuwa kupunga mkono kwako ama kujaribu kupiga kofi wadudu kunaweza kupunguza uwezekano wa wadudu hao kukuuma tena.

Watafiti hao kutoka chuo kikuu cha Washington cha Seattle wamebaini kuwa mbu wanaweza kujifunza na kutambua aina fulani ya harufu kupitia mshituko ama kofi.

Matokeo yake wataepuka harufu hiyo wakati mwingine.

“Pale mbu wanapobaini harufu za aina mbali mbali kwa njia ya kujilinda, harufu hizo huwafanya wachukue hatua sawa na wakati wanapopuliziwa dawa ya DEET, moja ya dawa ya kuua mbu,” alisema afisa wa ngazi ya juu ya uandishi wa utafiti huo Jeff Riffell, na profesa wa biolojia katika chuo kikuu cha Washington.

“Zaidi ya hayo, mbu hukumbuka harufu waliyozoweshwa kwa siku kadhaa

Watafiti tayari walikua wanafahamu kwamba mbu huwa wanachagia ni nani wa kumuuma na nani wasimuume.

Hivyo basi, kuna watu wanaopendelea kuwauma kuliko wengine.

Pia wanafahamika kwa kubadili makao kulingana na msimu, huku wakiwauma ndege msimu wa kiangazi na wanyama na ndege wakati wa majira mengine ya mwaka kwa mfano.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni