Afya

Utafiti:’Red Wine’ inaweza kukinga uozaji meno na ugonjwa wa fizi

Tarehe February 22, 2018

Mvinyo mwekundu awali ulihusishwa na faida mbali mbali za kiafya, kuanzia kusaidia kupunguza kihatari za kupata magonjwa ya moyo na na kisukari.

Sasa utafiti mpya unasema mvinyo huu una kemikali ambazo zinakabiliana na kuoza kwa meno na ugonjwa ufizi.

Watafiti walibaini kuwa mchanganyiko wa kemikali unaotengeneza kinywaji hicho, unaofahamika kama polyphenols, husaidia kumaliza kuwamaliza vimelea (bakteria) hatari kinywani.

Lakini watafiti hawa wanaonya kuwa matokeo ya utafiti wao hayatoi “ruhusa” ya kunywa mvinyo kupita kiasi.

Utafiti wa awali ulionnyesha kuwa faida za kiafya za polyphenols zilihusishwa na kuwa na uwezo wa kuulinda mwili dhidi ya vimelea hatari wanaoshambulia mwili.

Walibaini kuwa kemikali ya mvinyo na mvinyo kwa pamoja vilipunguza uwezo wa Bakteria wa kukaa kwenye seli, lakini kemikali zaa polyphenols – caffeic na p-coumaric acids – zilifanya kazi bora zaidi .

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni