Afya

Utafiti wabainisha njia bora kuepuka kujifungua mtoto aliyefariki

Tarehe November 20, 2017

Mmoja wa mama mjamzito.

Utafiti mpya  umewashauri  Wanawake  kulala kwa kutumia upande katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito wao ili kuzuia kujifungua watoto waliofariki tumboni.

Kwa mujibu ya  Utafiti huo,  zaidi ya wanawake 1000 ulibaini kuwa   hatari ya mtoto kufariki tumboni miongoni mwa wanawake wajawazito inaongezeka marudufu iwapo watalala kwa kutumia mgongo wao miezi mitatu ya mwisho katika ujauzito.

Utafiti huo ulichunguza mimba 291 zilizoharibika na wanawake 751 waliofanikiwa kupata watoto. Watafiti wanasema kuwa upande ambao wajawazito hulalia ni muhimu sana na kwamba hawafai kuwa na tashwishi yoyote wanapoamka na kugundua wamelalia migongo yao.

Takriban mimba 225 nchini Uingereza huishia mtoto kuharibika na watafiti wa utafiti huo wanakadiria kwamba takriban maisha ya watoto 130 kila mwaka yataokolewa iwapo wanawake wataendea kulala kwa kutumia upande wa kulia ama kushoto.

Utafiti huo wa MiNESS uliochapishwa katika jarida la Kujifungua ni mkubwa wa aina yake na unathibitisha tafiti ndogo nchini New Zealnd na Australia.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni