Afya

UTAFITI: Virusi vya ZIKA vinaweza kutibu saratani ya Ubongo

Tarehe September 7, 2017

Zika huathiri zaidi watoto wanaozaliwa.

Zika huathiri zaidi watoto wanaozaliwa.

Virusi hatari vinavyoweza kusababisha madhara kwa ubongo wa watoto, Zika vinaweza kusaidia kwenye matibabu mapya kwa saratani ya ubongo kwa mtu mzima, kwa mujibu wa wanasayansi nchini Marekani.

Hadi sasa virusi vya Zika vinaonekana kuwa tisho la afya duniani lakini utafiti wa hivi punde unaonyesha kuwa virusi hivi vinaweza kuvamia na kuua seli zinazosababisha saratani ya ubongo wa mtu mzima.

Majiribio yaliyofanywa kwa panya yalionyesha kuwa virusi vya Zika vilikula seli za saratani ya ubongo.

Binadamu bado hawajafanyiwa utafiti huo, lakini wataalamu wanaamini kuwa virusi hivyo vinaweza kuingizwa katika ubongo wa binadamu wakati wa upasuaji ili kuangamiza seli za saratani ya ubongo.

Pia matibabu hayo ya kutumia Zika yameonekana kufaulu kwenye sampuli za binadamu katika maabara.

Utafiti wa hivi karibuni kwa panya walio hai na kwa sampuli za binadamu unaonyesha kuwa matibabu ya kutumia Zika yanaweza kuua seli ambazo ni sugu kwa matibabu ya kipindi hiki.

Wanasayansi wa Uingereza katika chuo cha Cambridge nao wameanzisha utafiti sawa na huo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni