Afya

UTAFITI: Uzalishaji mbegu za kiume wapungua duniani

Tarehe July 26, 2017

_97076563_sperm

Utafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Hebrew-Hadassah Braun, cha Mjini Jerusalem umebaini kuwa kiwango cha mbegu za kiume kwa wanaume duniani kimepungua kwa zaidi ya asilimia 50.

Kwa mujibu wa utafiti huo, kiwango na ubora wa mbegu za kiume kimeshuka katika kipindi cha chini ya miaka 40 na hakuna ushahidi kuwa kiwango hicho kitaongezeka.

Utafiti huo umesisitiza kuwa kiwango na idadi ya mbegu za kiume kimeshuka zaidi kwa wanaume wa nchi za Magharibi huku pia zikidaiwa kushuka katika ubora na idadi na hivyo kuwa tishio kwa uwepo wa watu duniani.

“Utafiti huu unawapa wasomi kazi kubwa zaidi hasa kwani idadi ya mbegu za kiume na afya ya binadamu ni muhimu zaidi. Wasomi sasa wanatakiwa kuchunguza chanzo cha kushuka huko kwa idadi ya mbegu za kiume na namna ya kutatua tatizo hilo,” amesema mmoja wa watafiti hao, Dkt. Hagai Levine.

Dkt. Hagai ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mazingira na Afya wa Chuo cha Hebrew, amefanya utafiti huo kwa kushirikiana na Profesa Hannah Swan wa Chuo Kikuu cha New York, Kitengo cha Afya ya Jamii.

Madaktari wengine waliohusika katika utafiti huo ni wa kutoka nchi za Brazil, Denmark, Israel, Uhispania na Marekani.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni