Afya

Utafiti Sikika: ‘Dawa zinapatikana kwa urahisi Mahospitalini’

Tarehe August 1, 2017

Shirika lisilo la kiserikali la Sikika limebainisha kuridhishwa na upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya hapa nchini ambapo takwimu  zinaonesha kuimarika kupatikana kwa dawa  kutoka asilimia 56 kwa mwaka jana hadi kufikia asilimia 81 kwa mwaka huu.

Hayo yamekuja baada ya mazungumzo ya watendaji wa sikika wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika na  Wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari nchini katika ufuatiliaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma ya afya hapa nchini.

“Hiki ni kitu kikubwa ambacho hakijawahi kutokea kwa miaka mingi, kwamba kuna dawa kwa wingi na wananchi wanazipata kwa bei ile ile na kwa urahisi jambo kubwa kwao” alisema Kiria katika mazungumzo hayo.

Shirika hilo  limeishauri  Ofisi ya Rais Serikali,Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa(Tamisemi) kuendelea kuimarisha usimamizi  na matumizi ya dawa.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni