Afya

Ugonjwa wa Kaswende wadaiwa kuwa sugu kwa dawa

Tarehe July 7, 2017

Dalili za kaswende.

Dalili za kaswende.

Kaswende sasa inazidi kuwa ugonjwa sugu usiotibika hata kwa viuavijisumu (antibiotics), Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema.

“Bacteria wasababishao ugonjwa wa kaswende ni werevu sana. Kila mara tunapotumia viuavijisumu  kutibu maambukizi, ndivyo bacteria hao wanavyojibadili kukabiliana na viuavijisumu hivyo,” anasema Teodora Wi, mwakilishi wa WHO amesema.

Ametahadharisha kuwa watu wanapaswa kuwa makini kwakuwa tatizo hilo limezidi kuwa sugu kadiri siku zinavyozidi na vimelea (backteria)  waliopo hawawezi kuuliwa na dawa bora zilizopo sasa.

Wadudu watatu (vimelea) ambavyo haviwezi kuuliwa na dawa bora zipatikanazo sasa waligundulika nchini Japan, Ufaransa na Uhispania, kwa mujibu wa WHO.

“Kila mwaka watu zaidi ya Milioni 78 wanahisiwa kuambukizwa ugonjwa wa Kaswende,” WHO inasema.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni