Afya

Takwimu za Hali ya ukimwi nchini,Njombe bado kinara

Tarehe December 21, 2017

Takwimu inaonyesha  kuwa hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini mkoa wa Njombe ume endelea kuongoza ikifuatiwa na mikoa ya Mbeya na Iringa.

Dkt. Mpango amesema  kuwa  takwimu za utafiti uliofanywa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa juu ya hali ya maambukizi ya VVU,  inaonyesha kuwa Mkoa wa Njombe ndo unaoongoza kwa maambukizi  ya VVU, na utafiti huo uliwahusisha   watu wenye umri wa miaka 15-49 kwa mwaka 2016-17.

“Kiwango cha maambukizi mapya bado kiko juu kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania ikiongozwa na

Njombe 11.6%,

Iringa 11.2%

Mbeya 9.2%.

Mikoa yenye maambukizi ya kiwango cha chini ni

Unguja 0%,

Kaskazini Pemba 0%,

Lindi 0.3%,

Manyara 1.8%

Arusha 1.9%.”.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo Rais Magufuli amewataka wananchi kupuuzia watu wanaotoa takwimu za uongo, na kusema kwamba wenye mamlaka ya kutoa takwimu za taifa ni ofisi ya Taifa ya Takwimu pekee.

Ukimwi bado ni janga kubwa duniani na taifa kwa ujumla ambapo kundi la wanawake  ndilo lina kiwango cha juu cha maambukizi ya VVU.

Serikali imejiwekea mikakati kuhakikisha kuwa waliogundulika kuwa wameathirika wanaanzishiwa dawa, kuhimiza matumizi ya mpira wa kiume, kupunguza maambukizi mapya kwa asilimia 29 na kutoa elimu kwa wanawake wanaojihusisha na ngono, kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni