Afya

Serikali yatoa tahadhari kuenea ugonjwa wa Chikungunya

Tarehe January 21, 2018

Waziri wa Afya, Mh.Ummy Mwalimu.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa homa ya Chikungunya ambao umeripotiwa na vyombo vya habari kutokea jijini Mombasa nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu imesema kuwa mpaka sasa Shirika la Afya Duniani (WHO) bado haijatoa taarifa rasmi lakini wao wanaotoa taadhari kuzingatia muingiliano mkubwa wa watu baina ya nchini hizi mbili Kenya na Tanzania.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa ugonjwa wa Chikungunya unasababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa mbu wa aina ya Aedes na kusema ugonjwa huu si mgeni nchini Tanzania kwani ulishawahi kutokea.

Hadi sasa tiba ya ugonjwa huo bado haijagundulika, matibabu yake ni kwa ajili ya kupunguza makali ya dalili zake.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni