Afya

Serikali kuja na pedi za kutumika zaidi ya mara moja

Tarehe January 3, 2017

 

000000047

Serikali imesema kuwa inafanya tafiti mbalimbali ili kubaini na kuona kama kuna uwezekano wa kupata taulo za hedhi (pedi) ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha luninga nchini, Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla amesema mkakati huo ni katika kuhakikisha afya ya watoto wa kike inalindwa na kuepusha utoro mashuleni kutokana na tatizo la hedhi isiyo salama hasa maeneo ya vijijini na wale wasio na uwezo wa kuzipata taulo hizo.

“Sasa hivi tupo kwenye mchakato wa kuangalia zile pedi ambazo vijana wanaweza kutumia mwenzi mmoja, miwili hata mwaka mzima, hata kwa miaka miwili,” amesema Kigwangalla.

Amesema kuwa kuna nchi mbalimbali wameingiza kwenye soko bidhaa na namna hiyo kwa hiyo na Serikali inaendelea kuangalia tafiti mbalimbali kuhusu usalama wa hizi pedi ambazo unaweza kuzitumia kwa muda mrefu.

“Kwa hiyo tunaangalia kama na sisi tunaweza kuziruhusu kuingia nchini na sisi tuziingize sokoni. Lengo letu ni kuangalia usalama kwanza kabla hatujaziruhusu kutumika,” ameongeza.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni