Afya

Rais Duterte ataka masikini wote kupewa dawa za uzazi wa mpango

Tarehe January 12, 2017

_93536484_5dda98c4-2d74-44ae-94f3-f24930a21a3d

Mashirika ya kiserikali nchini Ufilipino yameamrishwa kutoa dawa bure za uzazi wa mpango kwa wanawake wapatao milioni sita ambao hawana uwezo wa kuzipata.

Rais Rodrigo Duterte amesema, anataka kupunguza idadi ya mimba zisizotakiwa, husususan ni miongoni mwa watu maskini.

Utekelezwaji wa amri yake hiyo unatarajiwa kukabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa kanisa katoliki la Roma.

Rais aliyekuwa madarakani kabla ya Bwana Duterte alipigania kupitishwa kwa muswada wa matumizi zaidi ya dawa za mpango wa uzazi nchini humo .

Hata hivyo mahakama kuu iliweka marufuku ya muda dhidi ya usambazaji dawa za kupanga uzazi chini ya sheria mwaka 2015 baada ya malalamiko kutoka kwa makundi yanayopinga utoaji mimba.

Zaidi ya 80% ya Wafilipino ni wafuasi wa kanisa Katoliki la Roma, kulingana na kituo cha utafiti cha Pew.

Msukumo wa kufanikiwa “kusambaza huduma ya mpango wa uzazi kwa kila mmoja “ni moja ya sehemu muhimu za mipango ya Wafilipino ‘ mipango ya kupunguza umaskini’, Waziri wa mipango ya kiuchumi Ernesto Pernia alinukuliwa na shirika la habari la Associated Press.

Serikali inataka kupunguza kiwango cha umaskini kwa 13% idikapo mwaka 2022, na ilifikiwa chini ya 21.6%mwkaa jana , aliongeza. Alisema kuwa serikali inaimani na faida za dawa za mpango wa uzazi “kwa kulinda maisha, kulinda haki za wanawake , watoto , na maendeleo ya uchumi”.

Idara ya elimu pia imeagizwa kutoa “elimu ya jinsia na yenye misingi ya haki kwa jinsia zote ” kuhusu uzazi katika shule , kulingana na ripoti za CNN kuhusu Ufilipino.

Ufilipino ni taifa pekee katika eneo la Asia- Pacific ambako viwango vya mimba za vijana wadogo vimeongezeka katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, kwa munibu wa Umoja wa Mataifa.

Nchi hiyo ina idadi ya watu wapatao milioni 103.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni