Afya

Nyama ya mbwa marufuku China

Tarehe May 19, 2017

Muandaaji wa nyama katika bucha ya nyama ya mbwa nchini Vietnam.

Muandaaji wa nyama katika bucha ya nyama ya mbwa nchini Vietnam.

Sherehe ya kula nyama ya mbwa nchini China ilio na umaarufu kwa ukatili wa wanyama mwaka huu itapigwa marufuku kuuza nyama ya mbwa.

Ulaji wa mbwa nchini China sio haramu na wauzaji wa nyama hiyo tayari wameanza kulalamikia marufuku hiyo wengine wakisema hawajaisikia. Sherehe hiyo inayofanyika mwezi Juni kila mwaka imekuwa ikivutia pingamizi kubwa kutoka kwa wanaharakati wa wanyama wanaosema kuwa wanyama hao hufanyiwa ukatili.

Inakadiriwa kuwa katika sherehe hiyo ya Yulin iliofanyika miaka michache iliopita, takriban mbwa na paka 10,000 walichinjwa na kufanywa kitoweo wakati wa sherehe hiyo ya siku kumi.

Lakini idadi hiyo imekuwa ikipungua katika siku za hivi karibuni huku pingamizi likiendelea nchini China. Wanaharakati kadhaa wa wanyama wanasema kuwa wauzaji na mikahawa wameambiwa kwamba hakuna nyama ya mbwa itakayouzwa wakati na kabla ya sherehe hiyo.

Peter Li, mtaalamu wa sera za China amesema mamlaka tayari imejaribu kuwakatisha tamaa wanaotekeleza hatua hiyo na kwamba mwaka huu itawapiga faini watakaokiuka marufuku hiyo.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni