Afya

Muhimbili yataja idadi ya watoto waliozaliwa Sikukuu ya Pasaka

Tarehe April 1, 2018

Jumla ya watoto 7 wamezaliwa siku ya leo Aprili Mosi, 2018, ambayo ni sikukuu ya pasaka, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Taarifa hiyo imetolewa na ofisi ya mahusiano ya hospitali ya Muhimbili, ambapo imeeleza kwamba watoto hao waliozaliwa wanne ni wa kike, huku wakiume wakiwa watatu, na wazazi sita wakiwa wamejifungua kawaida na mmoja kwa upasuaji.

Mama na watoto hao wote wapo salama na wanaendelea vizuri hospitalini hapo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni