Afya

MSD yadai upatikanaji wa dawa waimarika kwa asilimia 74

Tarehe January 11, 2017

msdpx-1

Bohari ya Dawa nchini imesema kuwa hali ya upatikanaji wa dawa kwasasa imeboreshwa kutoka asilimia 54 iliyokuwepo mwaka jana, hadi kufikia asilimia 74 hivi sasa.

Mkurugenzi MSD, Laurean Bwanakunu ameuhakikishia umma kuwa upatikanaji wa dawa utaimarika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu hadi kufikia asilimia 90.

Amesema kwa sasa kati ya aina za dawa muhimu 135 zinazohitajika kuwepo MSD dawa aina 100 zinapatika kwenye maghala ya MSD.

Amesema kuwa MSD imefanikiwa kurejesha maghala yaliyokuwa wamekodi kwa ajili ya kuhifadhia vifaa tiba, hatua ambayo inaokoa sh.Bilioni 4 ambazo zilikuwa zikilipwa kama kodi kila mwaka.

Ameongeza  kuwa MSD inatarajia kuzindua  duka la dawa la Mkoani Katavi, ambalo litaifanya MSD kuwa na jumla ya maduka Saba, mengine yakiwa mkoani Arusha, Dar es Salaam, Mwanza, Lindi, Geita naMbeya.

Akijibu swali juu ya ukosefu wa vifaa vyakujifungulia wajawazito Mkurugenzi Mkuu amesema vipo vyakutosha, na  zabuni ya manunuzi ya vifungashio kwa ajili ya vifaa hivyo vyakujifungulia iko katika mchakato wa kumpata mshitiri.

 

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni