Afya

Kinga mpya ya kupambana na HIV kwa asilimia 99 yaja

Tarehe September 22, 2017

Shirika la Kimataifa la Kukabiliana na Ukimwi ‘International Aids Society’ limesema kuwa ugunduzi wa kihistoria unakaribia baada ya wanasayansi kuendelea kutengeneza chembe chembe za kinga ya mwili zinazoweza kushambulia asilimia 99% ya virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi na hivyo kuzuia maambukizi kuendelea.

Chembe chembe hiyo ya kinga imetengenezwa kwa ajili ya kushambulia sehemu tatu muhimu za virusi na hivyo kuvifanya virusi hivyo kushindwa kuhimili mashambulizi yake.

Kazi ya utengenezaji chembe chembe hizo za kinga ya mwili imetokana na ushirikiano baina ya Taasisi ya Marekani ya Afya na kampuni Maduka ya Dawa ya Sanofi.

Majaribio ya kinga kinga hiyo ya mwili kwa binadamu yataanza kufanyika mwaka 2018 kuangalia kama dawa hiyo inaweza kuzuia ama kutibu maambukizi ya HIV.

“Miili yetu huhangaika kupigana na virusi vya HIV kwasababu virusi hivyo vina uwezo mkubwa wa kujibadilisha katika hali nyingine pamoja na muonekano wake,” wamesema wanasayansi hao.

Imedaiwa kuwa aina kadhaa za virusi vya HIV, katika mgonjwa mmoja zinaweza kufananishwa na zile za mafua wakati wa msimu wa baridi hivyo mfumo wa kinga ya mwili unajikuta katika vita dhidi ya magonjwa kadhaa nyemelezi yanayosababishwa na HIV.

Aidha, watafiti hao wamekuwa wakijaribu kutumia uwezo wa mwili wenyewe wa kupunguza uharibifu wa kinga ya mwili kama njia ya kutibu HIV, ama kuzuia maambukizi hayo mapema.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni