Afya

Hospitali zaaswa kotowauzia damu wagonjwa

Tarehe January 15, 2018

Serikali kupitia Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amezitaka Hospitali na vituo vya Afya nchini kuhakikisha wagonjwa hawauziwi damu.

Waziri Ummy amesema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuchangia damu ambayo inafanywa na Chama cha wanawake wa Tasnia ya Filamu nchini jijini Dar es salaam.

Akizungumza kwenye kampeni hiyo Ummy amesema damu haiuzwi na kwa mgonjwa yeyote atakayeuziwa damu kwenye kituo chochote cha afya cha Serikali atoe taarifa  kwenye idara husika na atachukuliwa hatua.

Aidha,amezitaka Hospitali na vituo vya Afya vya Serikali wahakikishe kuwa wanaweka matangazo yanayoelimisha wananchi kuwa damu haiuzwi bali inatolewa bila ya malipo

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni