Afya

Haya ndio Madhara ya matumizi ya Smartphone Kwenye Giza

Tarehe August 25, 2017

save image

 

Profesa Li Li, kiongozi wa hospitali ya macho nchini Singapore anasema mionzi ya moja kwa moja kwa zaidi ya dk 30 na kuendelea inaweza kusababisha mpangilio na mbadiliko wa seli macho na hivyo kusababisha saratani na kushindwa kuona kabisa.

Amesema wakati wa kutumia simu mahali penye giza huwa unayalazimisha macho yaweze kuona nje ya uwezo wake, ndio maaana kuna wakati unaweza ukatumia simu muda mrefu mahali penye giza mara baada ya kuacha kutumia simu utaona kama giza limezidi zaidi. Hali hiyo huyafanya macho yako yaanze kurudi katika hali ya ukawaida.

Simu za mikononi (smartphone) zenye mwanga mweupe sana karibu na macho gizani,hubadili mfumo wa seli za macho na kupelekea matatizo ya saratani ya macho.

Proffessor Li Li amesema dalili za mbadiliko wa seli macho mara nyingi hugunduliwa kwa  watu wenye umri mkubwa (wazee), ila kwa hivi sasa zinagunduliwa hata na kwa vijana wadogo. Hasa kwa wenye umri wa kuanzia miaka 30-40 wanaongezeka kwa asilimia 3% na wote hawa ni watumiaji wa simu za mikononi (smartphone) kupitiliza.

Utumiaji wa simu inaweza sababisha na ugonjwa wa macho makavu, mtoto wa jicho na mwisho kupelekea kupoteza kuona.

Maoni:

Ili kujikinga na Saratani ya Macho unapaswa kujiepusha na matumizi ya Smart phone gizani.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni