Afya

Chanjo ya ugonjwa wa Gonorrhoea yapatikana

Tarehe July 11, 2017

_96883578_aab941fa-44ac-4cc3-87f7-27a9993d79b4

Wanasayansi nchini New Zealand wameonyesha kwa mara ya kwanza kwamba kuna chanjo inayoweza kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa gonorrhoea.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Auckland wamegundua kuwa maambukizi ya ugonjwa huo wa zinaa yameshuka kwa takriban theluthi moja miongoni mwa watu ambao walipata chanjo dhidi ya homa ya manjano.

Watafiti hao wamefuatilia kutoka kwa vijana milioni moja waliopata chanjo hiyo pindi kulipotokea ugonjwa wa homa ya manjano nchini New Zealand.

Gonorrhoea imekuwa taabu kutibika kwa sababu imezoea viuavijisumu ‘antibiotics’.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya afya anasema utafiti huu unaonyesha inawezekana kuwa na chanjo dhidi ya ugonjwa huo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni