Afya

Bungeni:Halmashauri zatakiwa kuwa na chumba cha Watoto Njiti

Tarehe June 5, 2017

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Hamisi Kingwangalla akijibu hoja za wabunge.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezitaka halmashauri zote ambazo zinamiliki hospitali za wilaya kuhakikisha wana chumba maalum kwa ajili ya kuwapatia huduma maalum watoto  ambao wamezaliwa chini ya umri.

Akijibu hoja za wabunge leo Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Hamisi Kigwangalla amesema mkakati  wa serikali ni kuhakikisha hospitali zote za wilaya zina chumba maalum kwaajili ya kulea watoto waliozaliwa chini ya umri ili kuwepo kwa huduma maalum ya watoto hao.

Aidha amewaomba wabunge kutoa ushirikiano ili kuhakikisha huduma hiyo inapatikana katika wilaya zote.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni